
dream
108 posts







Mara nyingi ninapokutana na wazee au viongozi waliowahi kulitumikia taifa au chama hasa UVCCM au TYL (TANU Youth League) napenda sana kujifunza kutoka kwao, hasa kwa kusikiliza na kuuliza maswali. Siku moja, mzee Ulimwengu alitusimulia tukio ambalo lilinifurahisha na kunifundisha sana. Alieleza kwamba wakati fulani wakiwa bungeni, kulijitokeza tabia ya baadhi ya wabunge kutaka kuwahi kuondoka ili wakale nyama, hasa mwishoni mwa wiki. Hali hiyo ilisababisha wengine kuanza kuwaharakisha wabunge waliokuwa wanachangia kadri muda wa kikao ulivyokuwa unakaribia kuisha. Anasema siku moja aliposimama kuchangia, alimwomba Spika awaruhusu wale wanaotaka kwenda kula nyama waondoke, ili wabaki wale waliokuwa serious na masuala ya taifa waendelee kujadili mambo ya msingi. 😄😄🙌🏿💪🏿 Hiki ni kisa kimoja kati ya vingi kilichonifundisha sana, hasa ukizingatia alikuwa kiongozi ndani ya Jumuiya ya Vijana ya TANU. Heri ya kuzaliwa Mzee wetu watoto wako tunajifunza mengi kutoka kwako kupitia maandishi yako,simulizi zako,interviews zako nk. Mungu akujalie afya njema tuendelee kujifunza zaidi.






















