Burhani M. Mustapha (Mwagalazi)
33.6K posts

Burhani M. Mustapha (Mwagalazi)
@MustaphaBurhani
In Shaa Allah.





Mwandishi wa habari na mtetezi wa haki za binadamu, Devota Tweve, amechukua fomu ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Mbozi, mkoani Songwe, tarehe 29 Juni 2025, hatua inayotafsiriwa kama mwendelezo wa safari yake ya muda mrefu ya kutetea haki za watoto na wasichana nchini Tanzania. Devota @TweveDevota , anayejulikana kwa mchango wake mkubwa katika masuala ya kijamii, amewahi kutunukiwa Tuzo ya Umoja wa Mataifa ya Kujitolea kwa juhudi zake katika kufanikisha Malengo Endelevu ya Maendeleo (SDGs), hususan katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia. Pia ni mshindi wa Tuzo ya Kutokomeza Ukatili Mtandaoni iliyotolewa na shirika la WiLDAF kutokana na kampeni zake za kulinda usalama wa wanawake na wasichana katika majukwaa ya kidijitali. Kwa miaka mingi, Devota ameshirikiana na mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali kupigania haki za watoto, ikiwa ni pamoja na kupaza sauti dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia, kutetea haki ya wasichana waliopata mimba kurejea shule, kuelimisha jamii kuhusu usawa wa kijinsia na haki za binadamu. Kwa sasa, anataka kupeleka ajenda yake ya haki na usawa hadi kwenye ngazi ya maamuzi ya kitaifa kupitia nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Mbozi kupitia CCM, akiahidi kusimamia maendeleo jumuishi kwa wananchi wote.









Mungu sio Athumani hatimae kapona .















