lobos
1.7K posts

lobos
@takecaremate
Suspect is armed and dangerous, proceed with caution.





Mheshimiwa Jaji Mkuu kesi ya Lissu Mwanasheria Mkuu na timu yake wameona hawawezi kufanikiwa kumtia hatiani Lissu wameamua kuchelewesha kesi kuomba mapitio katika Mahakama ya Rufaa nayo imepaki kesi na mtaani vuguvugu la Free Lissu limeanza lawama ni Mahakama sio Mwanasheria Mkuu
















Jela sio sehemu salama, hakuna aliyekaa jela akabaki na msimamo wake uleule, Nampongeza Lissu kwakubadili msimamo wake na kuomba sasa maridhiano ya mezani, Ukikomaa utafia jela ndugu….. Waulize wapinzani wengine Afrika kilichowakuta. Yuko mtu kwasababu ya uelewa mdogo anaamini kuwa Marekani na Ulaya watakuja kumtoa Lissu pale Ukonga au watakuja kuitoa CCM madarakani na Lissu awe Rais. Hizo ni ndoto za chizi na kuota ndoto kwa kiumbe cha Mwenyezi Mungu sio dhambi…. Ulaya na Marekani wanaangalia maslahi yao, Vyovyote ccm na samia watakachowafanyia watz ilimradi maslahi ya Ulaya na Marekani hayaguswi basi sahauni ndoto zenu, mtaishia kupokea barua za matamko ya kulaani na kusisitiza amani na demokrasia tu. Nakujueni mnavichwa vigumu mtakomaza mafuvu yenu kubisha… Tulishauri tangu mwanzo kwamba tufanye siasa za maridhiano, tukawaambia kuwa hii ni kesi ya kisiasa, Siasa ndio imemweka jela Lissu, na Siasa ndio itamtoa jela Lissu, kwa lugha rahisi ni kwamba Lissu lindie kafanya Lissu aende jela, na Lissu ndie atafanya Lissu atoke jela. Kwakibri na jeuri ya umamuma wetu mlitutusi mkatuita wasaliti. Bahati nzuri Lissu akili imemjia kalitambua hili japo kwakuchelewa sana, Tumpongeze na tumtie moyo… karibuni kwenye siasa za kistaarabu za maridhiano kwa maslahi ya Tanzania yetu. Ushauri wangu kwa Serikali ni kwamba Mahakama iachwe ifanye kazi yake na haki ipatikane, Lissu atatukuta mbele tukiendelea na vikao vya maridhiano au atakuta nchi ilisharidhiana inaendelea vizuri na atafaidi matunda ya maridhiano. Na Yericko Nyerere
























