Damas Damian Kawonga
1.3K posts

Damas Damian Kawonga
@DAMASDAMIANKAWO
If you don't stand for something, you will fail for anything
















Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka amesema serikali inaendelea na utafiti wa kuanzisha Benki ya Vijana itakayolenga kutoa huduma za kifedha zinazokidhi mahitaji ya vijana Nchini. Amesema hayo wakati akiwasilisha hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/27, akieleza kuwa hatua hiyo inalenga kuweka msingi imara wa taasisi maalum ya kifedha itakayowawezesha Vijana kupata mitaji kwa urahisi. “Dhamira ya Serikali ni kuweka msingi wa mfumo wa kifedha unaoendana na mazingira na uwezo wa vijana wengi, hususan wale wanaoanza shughuli za kiuchumi, ili kuondoa vikwazo vilivyopo katika upatikanaji wa mitaji. Benki ya Vijana, itakayoanzishwa, itakuwa chombo muhimu cha kimkakati kitakachowezesha upatikanaji wa huduma za kifedha zilizo rafiki kwa vijana, kuchochea ubunifu wa bidhaa za kifedha zinazolingana na mahitaji yao, kupanua wigo wa uwekezaji wa vijana, na hatimaye kuongeza ajira na mchango wa vijana katika kukuza uchumi shindani na jumuishi wa Taifa,” Mhe. Nanauka - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana. #MillardAyoUPDATES


















