
PLeaBargain
1.1K posts




Kwa vyovyote itakavyotolewa na kusema Tume ya Jaji Chande Othmani Juu ya Vurugu na Mauaji ya October 29, 2025 ni batili na haramu tokea ilipoundwa. Kwa sababu zifuatazo: 1. Imeundwa na Samia Suluhu Hassani ambaye ndiye mtuhumiwa namba Moja kwani ndiye alitoa amri ya kuwapiga risasi waandamanaji na watu ambao hawakuwa waandamanaji. 2. Samia alisema wakati wa Kampeni haramu za Udanganyifu Mkuu kuwa wanaosema hakutakuwa na uchaguzi wakumbuke kuwa yeye ndiye Amiri Jeshi Mkuu na kuwa hakutakuwa na nywinywi wala nywinywinywi. 3. Waandamanaji hawakuwa na silaha za moto ajabu yake walipigwa risasi kinyume kabisa na taratibu za kimataifa na nchi yetu za kukabiliana na waandamanaji ambazo ni matumizi ya mabomu ya machozi, maji ya kuwashawasha, hewa ya pilipili na ikilazimika risasi za plastiki. 4. Kuwekwa kwa zuio la kutoka nje na kutembea lililotangazwa na IGP Camillius Wambura ilikuwa kinyume Cha Sheria kwani hana mamlaka hayo. 5. Kuzimwa Kwa mtandao wa intaneti kwa siku sita ilikuwa kinyume Cha Sheria. Kwa kuzimwa kwake mauaji mengi yalitokea na yalisababisha watu kutokupata taarifa za kiwakati juu ya maovu makubwa yaliyofanywa na vyombo hivyo vya dola. 6. Kuzimwa kwa mtandao na zuio la kutoka nje sehemu nyingi za nchi yetu ilimaanisha hata wafanyakazi na mawakala wa Tume ya Udanganyifu Mkuu ya Jacobs Mwambegele haikuwa na uwezo wa kupata matokeo ya uchaguzi huo haramu. Ajabu yake Mdanganyifu huyo Mkuu asiyeheshimu kazi na maadili ya ujaji akatangaza matokeo kama kwamba uchaguzi ulifanyika na kura kuhesabiwa na matokeo kutangazwa katika Kila kituo na hatimaye kutumwa kwa Tume hiyo haramu! 7. Stargomena Tax ambaye alikuwa Waziri wa Ulinzi katika serikali ya Samia wakati wa udanganyifu huo ni mjumbe katika Tume hiyo ya Chande! Ni kanuni ya kisheria na haki kuwa huyu ana mgogoro wa kimaslahi na ni sehemu ya waliopaswa kuchunguza imekuwaje akageuka kuwa mchunguzi. 8. Jaji Othmani Chande na Jaji Ibrahimu Juma wanajua, kama wajuavyo wanasheria na wasomi wote, kuwa huwezi ukawa hakimu au muamuzi katika kesi yako mwenyewe(Nemo judex in causa sua) sasa imekuwaje wawe katika Tume ambayo ina kasoro hii kubwa? Je, si inafahamika kuwa pale Tume inapokuwa na kasoro hiyo yote iliyoyafanya hata kama ni mazuri, kisheria Huwa batili? 9. Wakati Tume inaanza kazi Samia ametoa matamshi ya kuingilia kati au kutoa majibu kwa Time ikiwa ni pamoja na kusema "nguvu iliyotumika ilikuwa sahihi" na kuwa "kwa nini wazazi hamkuwazuia watoto wenu kutoka nje?". Sasa hapo nini kinachunguzwa? 10. Tume ilizuia uwazi wa watu waliotoa maelezo yao kwa kuvikataza vyombo vya habari kuendelea kutoa maelezo ya waathirika wa mauaji hayo ya kinyama yaliyofanywa na vyombo vya dola. Kukosekana kwa uwazi ulikuwa mkakati wa kuleta giza na kuzuia ukweli wa mauaji hayo kufahamika na hivyo kile kitakachosemwa na Tume kuwa eti ndicho kilichosemwa na waathirika kichukuliwe kuwa ni cha ukweli. 11. Tume yenyewe imeanza kampeni ya kuuandaa umma kupokea ripoti yake na imekuwa na wasemaji wake. Hiyo inaashiria nia mbaya ya Tume hiyo. Ni kwa msingi na sababu hizo nasema kuwa Tume hiyo ni batili na chote kitakochotolewa nayo ni batili.















Umoja wa Wasafirishaji Abiria Dar es Salaam (UWADAR) umeomba kusitisha kutoa huduma kutokana na kujiendesha kwa hasara tangu kutangazwa kwa ongezeko la gharama za mafuta.


Commission probing Tanzania election violence gets fresh extension to April 24 thecitizen.co.tz/tanzania/news/…























